تَٱللَّهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ أَعْمَٰلَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini Shetani akawapambia matendo yao. Kwa hivyo leo, yeye ndiye kipenzi chao msaidizi, nao wana adhabu chungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako,lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata adhabu chungu.