وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْجِبَالِ أَكْنَٰنًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلْحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anavyowatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu amekufanyieni vivuli katika vitu alivyo viumba,na amekufanyieni maskani milimani, na amekufanyieni nguo za kukingeni na joto, na nguo za kukingeni katika vita vyenu. Ndio hivyo anakutimizieni neema zake ili mpate kut'ii.