ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَمَن رَّزَقْنَٰهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا هَلْ يَسْتَوُۥنَ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliyemruzuku riziki njema inayotoka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi (sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu)! Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliye mruzuku riziki njema inayo toka kwetu,naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhaahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu.Lakini wengi wao hawajui.