Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetakasika yule aliyemsafirisha mja wake usiku mmoja kutoka katika Msikiti Mtakatifu mpaka Msikiti wa Al-Aqswa, ambao tumebariki kandoni mwake, ili tumuonyeshe katika Ishara zetu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia zaidi, Mwenye kuona mno.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimpa Musa Kitabu na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawaambia) kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mtegemewa wenu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba hakika mtafanya uharibifu katika ardhi mara mbili, na hakika mtapanda kiburi, kupanda kukubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa itakapokuja ahadi ya kwanza yake, tutawatumia waja wetu wenye nguvu kubwa. Watawaingilia ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawarudishia nguvu zenu dhidi yao, na tukawasaidia kwa mali na wana, na tukawafanya kuwa wengi zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMkifanya wema, mnafanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu na waingie Msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni, na mkirudia, na sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannam kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hii Qur-ani inaongoa kwenye yale yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba wana malipo makubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na ili mpate kujua idadi ya miaka na hesabu. Na kila kitu tumekifafanua kwa kina waziwazi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila mtu tumemfungia matendo yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta ki wazi kimekunjuliwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayeongoka, basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anayepotea, basi anapotea kwa hasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumtume mtume.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pindi tukitaka kuuteketeza mji, tunawaamrisha wale wana starehe na taanusi wake, lakini wao wakaendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli ikathibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuhu! Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja wake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayetaka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea humo (duniani) tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu, ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anayeitaka Akhera, na akaifanyia juhudi ipasavyo ilhali ni Muumini, basi hao juhudi zao zitakuwa ni za kushukuriwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWote hao tunawakunjulia, hawa na hao, katika vipawa vya Mola wako Mlezi. Wala vipawa vya Mola wako Mlezi havizuiliki.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAngalia vipi tulivyowafadhilisha baadhi yao kuliko wengine wao. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata, "Ah!" Wala usiwakemee. Na uwaambie maneno ya heshima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wenu Mlezi anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanaorudi sana kwake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona vyema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao kulikuwa ni kosa kubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipokuwa kwa haki. Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa, basi hakika tumempa msimamizi wake mamlaka. Lakini asipitilize kiasi katika kuua. Kwani yeye anasaidiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiyakaribie mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo nzuri zaidi, mpaka afike utu uzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usiyafuate usiyo na elimu nayo. Hakika kusikia, na kuona, na (ufahamu wa) moyo hivyo vyote itaulizwa juu yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usitembee katika ardhi kwa kiburi. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi na kamwe huwezi kufikia urefu wa milima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni katika hekima alizokufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, ukaja ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumekwishabainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterZinamtakasa mbingu zote saba na ardhi na vyote vilivyo ndani yake. Na hakuna kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapomtaja katika Qur-ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakaenda zao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Ni nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Ni lini hayo? Sema: Labda huenda itakuwa hivi karibuni!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine, na Daudi tulimpa Zaburi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ambao wao wanawaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno, na wanataraji rehema zake, na wanaihofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakuna mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwishaandikwa katika Kitabu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakuna kinachotuzuia kutuma miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatutumii Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuhofisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Hebu unamuona huyu uliyemtukuza zaidi yangu, ukiniahirisha mpaka Siku ya Kiyama, hapana shaka nitakiangamiza kizazi chake isipokuwa wachache tu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shetani hawapi ahadi isipokuwa ya udanganyifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wenu Mlezi ndiye anayewaendeshea merikebu katika bahari ili mtafute katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa kukurehemuni.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa inapowakuta taabu katika bahari, hao mnaowaomba wanapotea, isipokuwa Yeye tu. Na anapowaokoa mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanadamu ni mwingi wa kukufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mna amani ya kuwa hatawadidimiza katika upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatawatumia tufani la kokoto? Kisha msipate yeyote wa kumtegemea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu mna amani ya kuwa hatawarudisha humo mara nyingine na akawatumia kimbunga cha upepo akawazamisha kwa mlivyokufuru, na kisha msipate wa kuwanusuru kutokana nasi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumewatukuza wanadamu, na tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na tukawaruzuku katika vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa wale tuliowaumba.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku tutakapoita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho, basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapo basi bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSimamisha Swala jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Qur-ani ya alfajiri. Hakika Qur-ani ya alfajiri inashuhudiwa daima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa amka usiku kwa ajili ya kufanya ibada kwayo, ni ziada ya sunna hasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinachosifika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunateremsha katika Qur-ani yale ambayo ni uponyaji na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu isipokuwa hasara.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi yule aliyeongoka katika njia."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuuliza habari za Roho. Sema, "Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika elimu isipokuwa kidogo tu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawawezi kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana wao kwa wao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano. Lakini wengi wa watu wakakataa isipokuwa kukufuru tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu uwe na nyumba iliyopambwa, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome.ˮ Sema, “Subhana Rabbi (Ametakasika Mola wangu Mlezi)! Kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu Mtume?"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakikuwazuilia watu kuamini ulipowajia uongofu isipokuwa ni kwamba walisema, "Je, Mwenyezi Mungu alimtuma mtu kuwa ni Mtume?"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoa, basi huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye anampotoa, basi hutawapatia walinzi wowote badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao, huku ni vipofu, mabubu, na viziwi. Na makazi yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu, na wakasema: Hivyo tukishakuwa mifupa na mapande yaliyovurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukufuru tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Lau kuwa nyinyi mnazimiliki hazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngelizuia kwa sababu ya kuhofu kuzitumia. Na mtu tangu hapo tabia yake ni mchoyo mno!"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Basi waulize Wana wa Israili alipowafikia, na Firauni akamwaambia, "Hakika mimi ninakuona wewe Musa umerogwa!"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akasema, "Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa utaangamizwa."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha majini yeye na wale waliokuwa pamoja naye wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawaambia baada yake Wana wa Israili, "Kaeni katika nchi. Na itakapokuja ahadi ya Akhera, tutawaleta nyote pamoja."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Iaminini au msiiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Hakika, Yeye ana majina mazuri zaidi." Wala usiswali Swala yako kwa sauti kubwa sana, wala usiifiche kwa sauti ndogo sana, bali shika njia ya kati na kati ya hizo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Alhamdulillah (sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme, wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.