مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُۥ مُطْمَئِنٌّۢ بِٱلْإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini yule aliyekifungulia kifua chake ukafiri - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao wana adhabu kubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAnaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa.