caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Qamar القمر

Aya 55 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 37

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٱقْتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلْقَمَرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSaa imekaribia, na mwezi umepasuka!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن يَرَوْا۟ ءَايَةً يُعْرِضُوا۟ وَيَقُولُوا۟ سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakiona Ishara, hugeuka upande na husema: 'Huu uchawi tu unazidi kuendelea.'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَّبُوا۟ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُمْ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّنَ ٱلْأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka zimewajia habari zenye makaripio.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حِكْمَةٌۢ بَٰلِغَةٌ فَمَا تُغْنِ ٱلنُّذُرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHekima kamili; lakini maonyo hayafai kitu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ يَوْمَ يَدْعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَىْءٍ نُّكُرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi jiepushe nao. Siku atakapoita mwitaji kuliendea jambo linalochusha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خُشَّعًا أَبْصَٰرُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMacho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige waliotawanyika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مُّهْطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِ يَقُولُ ٱلْكَٰفِرُونَ هَٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: 'Hii ni siku ngumu.'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا۟ عَبْدَنَا وَقَالُوا۟ مَجْنُونٌ وَٱزْدُجِرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَغْلُوبٌ فَٱنتَصِرْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: 'Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَفَتَحْنَآ أَبْوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٍ مُّنْهَمِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayomiminika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَفَجَّرْنَا ٱلْأَرْضَ عُيُونًا فَٱلْتَقَى ٱلْمَآءُ عَلَىٰٓ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukazipasua ardhi kwa chemichemi, yakakutana maji kwa jambo lililokwisha pangwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَحَمَلْنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَٰحٍ وَدُسُرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukambeba kwenye safina ya mbao na kamba.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَجْرِى بِأَعْيُنِنَا جَزَآءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIkawa inakwenda kwa macho yetu, kuwa ni malipo kwa aliyekuwa amekanushwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَد تَّرَكْنَٰهَآ ءَايَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKina 'Adi walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِى يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tuliwatumia upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUkiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilivyong'olewa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anayekumbuka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterThamudi waliwakanusha Waonyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالُوٓا۟ أَبَشَرًا مِّنَّا وَٰحِدًا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذًا لَّفِى ضَلَٰلٍ وَسُعُرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: 'Ati tumfuate binadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotovu na kichaa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَءُلْقِىَ ٱلذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنۢ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mno, mshari mkubwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ ٱلْكَذَّابُ ٱلْأَشِرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKesho watajua ni nani huyo mwongo mno, mshari mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا مُرْسِلُوا۟ ٱلنَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَٱرْتَقِبْهُمْ وَٱصْطَبِرْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tutawatumia ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame vyema tu na ustahamili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ ٱلْمَآءَ قِسْمَةٌۢ بَيْنَهُمْ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waambie kwamba hakika maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliyehusika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَنَادَوْا۟ صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَكَانُوا۟ كَهَشِيمِ ٱلْمُحْتَظِرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tuliwatumia ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea ua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍۭ بِٱلنُّذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ نَّجَّيْنَٰهُم بِسَحَرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tukawatumia kimbunga cha vijiwe, isipokuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا كَذَٰلِكَ نَجْزِى مَن شَكَرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa neema inayotoka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anayeshukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَنذَرَهُم بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا۟ بِٱلنُّذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِۦ فَطَمَسْنَآ أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: 'Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ صَبَّحَهُم بُكْرَةً عَذَابٌ مُّسْتَقِرٌّ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi onjeni adhabu na maonyo yangu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumeisahilisha Qur-ani kuikumbuka. Lakini yupo anayekumbuka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ جَآءَ ءَالَ فِرْعَوْنَ ٱلنُّذُرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Waonyaji waliwajia watu wa Firauni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَٰهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُو۟لَٰٓئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَآءَةٌ فِى ٱلزُّبُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ndiyo wanasema: 'Sisi ni wengi tutashinda tu.'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيُهْزَمُ ٱلْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَٱلسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali Saa ya Kiyama ndiyo miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلْمُجْرِمِينَ فِى ضَلَٰلٍ وَسُعُرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wakosefu wamo katika upotovu na wazimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِى ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا۟ مَسَّ سَقَرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku watakapokokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: 'Onjeni mguso wa Saqar!'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كُلَّ شَىْءٍ خَلَقْنَٰهُ بِقَدَرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَمْرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٌ كَلَمْحٍۭ بِٱلْبَصَرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَآ أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anayekumbuka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكُلُّ شَىْءٍ فَعَلُوهُ فِى ٱلزُّبُرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila jambo walilolifanya limo vitabuni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُّسْتَطَرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّٰتٍ وَنَهَرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na mito.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika mahali pa kukalia pa haki kwa Mfalme Mwenye uweza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70