caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Najm النجم

Aya 62 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 23

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNinaapa kwa nyota inapotua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلْهَوَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hatamki kwa matamanio.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْىٌ يُوحَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلْقُوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmemfundisha aliye Mwingi wa nguvu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذُو مِرَّةٍ فَٱسْتَوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kutua, akatulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ بِٱلْأُفُقِ ٱلْأَعْلَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye yuko juu kabisa upeo wa macho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akakaribia na akateremka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَوْحَىٰٓ إِلَىٰ عَبْدِهِۦ مَآ أَوْحَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alichomfunulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَذَبَ ٱلْفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUfahamu wa moyo wake haukukanusha uliyoyaona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mnabishana naye kwa aliyoyaona?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ رَءَاهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akamwona mara nyingine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عِندَ سِدْرَةِ ٱلْمُنتَهَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterPenye Mkunazi wa mwisho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عِندَهَا جَنَّةُ ٱلْمَأْوَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKaribu yake ndiyo ipo Bustani ya mbinguni inayokaliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ يَغْشَى ٱلسِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKilipoufunika huo Mkunazi hicho kilichoufunika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا زَاغَ ٱلْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلْكُبْرَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَرَءَيْتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلْعُزَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mmemuona Lata na Uzza?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلْأُخْرَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Manaat, mwingine wa tatu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلْأُنثَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuo ni mgawanyo wa dhuluma!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هِىَ إِلَّآ أَسْمَآءٌ سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَٰنٍ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهْوَى ٱلْأَنفُسُ وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلْهُدَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo hayakuwa ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ لِلْإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti mtu anakipata kila anachokitamani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلِلَّهِ ٱلْـَٔاخِرَةُ وَٱلْأُولَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye Akhera na dunia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغْنِى شَفَٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعْدِ أَن يَأْذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرْضَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةَ تَسْمِيَةَ ٱلْأُنثَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wasioamini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًٔا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao hawana elimu yoyote kwa hayo isipokuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mwachilie mbali anayeupa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱهْتَدَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuo ndio mwisho wao wa elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anayemjua zaidi mwenye kuongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ بِٱلْحُسْنَى

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo mbinguni na vilivyo katika ardhi, ili awalipe wale waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na wale waliotenda mema awalipe mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلْإِثْمِ وَٱلْفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلْمَغْفِرَةِ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِى بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمْ فَلَا تُزَكُّوٓا۟ أَنفُسَكُمْ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanajiweka mbali na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipokuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijione watakatifu. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga akawa mbali na maovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَرَءَيْتَ ٱلَّذِى تَوَلَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, umemwona yule aliyegeuka akaenda zake?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akapeana kidogo, kisha akajizuia?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِى صُحُفِ مُوسَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِبْرَٰهِيمَ ٱلَّذِى وَفَّىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa kwamba hakika nafsi iliyobeba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّ سَعْيَهُۥ سَوْفَ يُرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba vitendo vyake vitaonekana?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ يُجْزَىٰهُ ٱلْجَزَآءَ ٱلْأَوْفَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha ndio atalipwa malipo yake kwa hayo kwa ukamilifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba kwa Mola wako Mlezi ndiyo mwisho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba Yeye ndiye anayefisha na kuhuisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba Yeye ndiye aliyeumba jozi, dume na jike.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّ عَلَيْهِ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُخْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba ni Yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُۥٓ أَهْلَكَ عَادًا ٱلْأُولَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba Yeye ndiye aliyewaangamiza 'Adi wa kwanza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَثَمُودَا۟ فَمَآ أَبْقَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Thamudi hakuwabakisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhalimu zaidi, na waovu zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miji iliyopinduliwa, ni Yeye aliyeipindua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVikaifunika vilivyofunika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi neema gani ya Mola wako Mlezi unayoifanyia shaka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلْأُولَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHili ni onyo katika maonyo yale yale ya zamani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَزِفَتِ ٱلْـَٔازِفَةُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKiyama kimekaribia!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapana wa kukifichua isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمِنْ هَٰذَا ٱلْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mnayastaajabia maneno haya?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnacheka, wala hamlii?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنتُمْ سَٰمِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNanyi mmeghafilika?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ وَٱعْبُدُوا۟

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70