Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kuwa na mwana, basi bila ya shaka angeliteua amtakaye katika aliowaumba. Ametakasika na hayo! Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilichowekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmewaumba kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akawaletea wanyama wa mifugo jozi nane. Anawaumba katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa taabu inapomfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyokuwa akimwomba zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu mbali na njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi... Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika wanaokumbuka ni watu wenye akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi waja wangu mlioamini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYatawekwa juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora yake. Hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini waliomcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchemi katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbalimbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotovu wa dhahiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, atakayekuwa anapambana kwa uso wake na adhabu mbaya kabisa Siku ya Kiyama, (ni sawa na watenda wema?) Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangelijua!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana, na wa mtu mwingine aliyehusika na bwana mmoja tu. Je, wako sawa katika hali zao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uongo Mwenyezi Mungu na akaukadhibisha ukweli ulipomfikia? Je, siyo katika Jahannamu makazi ya hao makafiri?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu walioufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasiokuwa Yeye! Na aliyepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi hana wa kumpotoa. Je, Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu, anayeweza kulipiza?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukiwauliza: Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je, mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye na wategemee wanaotegemea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, ni kwa faida ya nafsi yake. Na mwenye kupotoka, bila ya shaka amepotoka kwa hasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa. Na zile zisizokufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizohukumiwa kufa, na huzirudisha nyingine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ndio wanachukua waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi wao hufurahi mno.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa wale waliodhulumu wangelikuwa na vyote vilivyomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikomboa kutokana na adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatarajia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu. Sivyo! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ukawasibu uovu wa yale waliyoyachuma. Na wale waliodhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa yale waliyoyachuma vile vile. Nao si wenye kushinda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye kumcha Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Siku ya Kiyama utawaona waliomsingizia uongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je, si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utakaowagusa, wala hawatahuzunika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale waliozikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kuhasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wala hawakumheshimu Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuheshimiwa. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kiume. Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapoifikia, itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliomcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapofikia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Amani iwe juu yenu! Mmetahirika. Basi ingieni humu mkae milele.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao watasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote!