caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Qasas القصص

Aya 88 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 49

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ طسٓمٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTwa Sin Mim.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تِلْكَ ءَايَٰتُ ٱلْكِتَٰبِ ٱلْمُبِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نَتْلُوا۟ عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِٱلْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTunakusomea katika habari za Musa na Firauni kwa Haki kwa ajili ya watu wanaoamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Firauni alitakabari katika ardhi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha hai watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika waharibifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ ٱلْوَٰرِثِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَنُرِىَ فِرْعَوْنَ وَهَٰمَٰنَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَحْذَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kuwaimarisha katika ardhi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyokuwa wakiyaogopa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰٓ أُمِّ مُوسَىٰٓ أَنْ أَرْضِعِيهِ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِى ٱلْيَمِّ وَلَا تَخَافِى وَلَا تَحْزَنِىٓ إِنَّا رَآدُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapomhofia, basi mtie mtoni, na usihofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلْتَقَطَهُۥٓ ءَالُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَٰمَٰنَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا۟ خَٰطِـِٔينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَتِ ٱمْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّى وَلَكَ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوْ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkewe Firauni alisema, "Atakuwa kiburudisho cha macho yangu na yako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu." Wala wao hawakutambua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَٰرِغًا إِن كَادَتْ لَتُبْدِى بِهِۦ لَوْلَآ أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa (ufahamu wa) moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingelikuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَتْ لِأُخْتِهِۦ قُصِّيهِ فَبَصُرَتْ بِهِۦ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye akamwambia dada yake Musa, "Mfuatie." Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali bila ya wao kujua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ ٱلْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰٓ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُۥ لَكُمْ وَهُمْ لَهُۥ نَٰصِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo. Kwa hivyo, dada yake akasema, "Je, niwaonyesheni watu wa nyumba watakaomlelea huyu, nao pia watakuwa wema kwake?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَرَدَدْنَٰهُ إِلَىٰٓ أُمِّهِۦ كَىْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُۥ وَٱسْتَوَىٰٓ ءَاتَيْنَٰهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa alipofika utu uzima barabara, tulimpa akili na elimu. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَدَخَلَ ٱلْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَٰذَا مِن شِيعَتِهِۦ وَهَٰذَا مِنْ عَدُوِّهِۦ فَٱسْتَغَٰثَهُ ٱلَّذِى مِن شِيعَتِهِۦ عَلَى ٱلَّذِى مِنْ عَدُوِّهِۦ فَوَكَزَهُۥ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ قَالَ هَٰذَا مِنْ عَمَلِ ٱلشَّيْطَٰنِ إِنَّهُۥ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo wanaume wawili wanapigana - mmoja ni katika watu wake, na mwingine katika maadui zake. Kwa hivyo, yule wa kutoka kwa watu wake akamtaka msaada kumpiga adui yake. Kwa hivyo, Musa akampiga ngumi, na akamuua. Akasema, "Hiki ni katika kitendo cha Shetani. Hakika yeye ni adui, mpotezaji dhahiri."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى فَٱغْفِرْ لِى فَغَفَرَ لَهُۥٓ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nimejidhulumu mwenyewe. Basi nisamehe." Kwa hivyo, akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَنْعَمْتَ عَلَىَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Mola wangu Mlezi, kwa yale uliyonineemesha, basi mimi sitakuwa kabisa msaidizi wa wahalifu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَصْبَحَ فِى ٱلْمَدِينَةِ خَآئِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا ٱلَّذِى ٱسْتَنصَرَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُۥ قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰٓ إِنَّكَ لَغَوِىٌّ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkapambazukiwa mjini asubuhi naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliyemtaka msaada jana akawa anamuita kwa sauti kubwa amsaidie. Musa akamwambia, "Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّآ أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِٱلَّذِى هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِى كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًۢا بِٱلْأَمْسِ إِن تُرِيدُ إِلَّآ أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلْمُصْلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipotaka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema, "Ewe Musa, unataka kuniua kama ulivyomuuwa mwanamume jana? Wewe hutaki isipokuwa kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wale watengenezao mambo."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَآءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّ ٱلْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَٱخْرُجْ إِنِّى لَكَ مِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaja mbio mwanamume mmoja kutoka sehemu ya mbali mno ya mji, akasema, "Ewe Musa! Hakika, wakubwa wanashauriana juu yako kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَخَرَجَ مِنْهَا خَآئِفًا يَتَرَقَّبُ قَالَ رَبِّ نَجِّنِى مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akatoka humo, naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Akasema, "Mola wangu Mlezi, niokoe kutokana na watu hawa madhalimu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَآءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يَهْدِيَنِى سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipoelekea upande wa Madyana, alisema, "Huenda Mola wangu Mlezi akaniongoa njia iliyo sawa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَمَّا وَرَدَ مَآءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ ٱلنَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ ٱمْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا قَالَتَا لَا نَسْقِى حَتَّىٰ يُصْدِرَ ٱلرِّعَآءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipoyafikia maji ya Madyana, akakuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema, "Mna nini?" Wakasema, "Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachungaji. Na baba yetu ni mzee sana."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّى لِمَآ أَنزَلْتَ إِلَىَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَجَآءَتْهُ إِحْدَىٰهُمَا تَمْشِى عَلَى ٱسْتِحْيَآءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِى يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا فَلَمَّا جَآءَهُۥ وَقَصَّ عَلَيْهِ ٱلْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ نَجَوْتَ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema, "Hakika baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea." Basi alipomjia na akamsimulia visa vyake, alisema, "Usihofu; umekwishaokoka kutokana na watu hao madhalimu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَتْ إِحْدَىٰهُمَا يَٰٓأَبَتِ ٱسْتَـْٔجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ ٱسْتَـْٔجَرْتَ ٱلْقَوِىُّ ٱلْأَمِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema mmoja katika wale wanawake, "Ewe baba yetu, muajiri huyu. Hakika mbora zaidi unayeweza kuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنِّىٓ أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ٱبْنَتَىَّ هَٰتَيْنِ عَلَىٰٓ أَن تَأْجُرَنِى ثَمَٰنِىَ حِجَجٍ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ وَمَآ أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Hakika mimi ninataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa sharti kwamba unitumikie miaka minane. Lakini ukitimiza kumi, basi hiari ni yako. Nami sitaki kukutaabisha. Mwenyezi Mungu akipenda (Inshallah), utanikuta miongoni mwa watu wema."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِى وَبَيْنَكَ أَيَّمَا ٱلْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَٰنَ عَلَىَّ وَٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akasema, "Hayo yamekwisha kuwa baina yangu na wewe. Muda mmojapo nikiumaliza, sitiwi ubayani. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa juu ya haya tunayoyasema."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى ٱلْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِۦٓ ءَانَسَ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ ٱمْكُثُوٓا۟ إِنِّىٓ ءَانَسْتُ نَارًا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ ٱلنَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Musa alipotimiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima 'Turi. Akawaambia ahali zake, "Ngojeni! Hakika mimi nimeona moto. Labda nitawaletea kutoka huko habari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِىَ مِن شَٰطِئِ ٱلْوَادِ ٱلْأَيْمَنِ فِى ٱلْبُقْعَةِ ٱلْمُبَٰرَكَةِ مِنَ ٱلشَّجَرَةِ أَن يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّىٓ أَنَا ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipoufikia, aliitwa kutokea ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lililobarikiwa kutoka kwenye mti, "Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ يَٰمُوسَىٰٓ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ إِنَّكَ مِنَ ٱلْـَٔامِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tupa chini fimbo yako. Basi alipoiona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma wala hakutazama. (Akaambiwa), "Ewe Musa, njoo mbele wala usihofu. Hakika wewe ni miongoni mwa walio katika amani."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱسْلُكْ يَدَكَ فِى جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَآءَ مِنْ غَيْرِ سُوٓءٍ وَٱضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ ٱلرَّهْبِ فَذَٰنِكَ بُرْهَٰنَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦٓ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIngiza mkono wako kwenye mfuko wako, utatoka mweupe pasipo na ubaya wowote. Na jiambatishe mkono wako ukihisi hofu. Basi hizi ni hoja mbili zitokazo kwa Mola wako Mlezi umpelekee Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ إِنِّى قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nilimuua mtu katika wao, kwa hivyo ninahofu wataniua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَخِى هَٰرُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّى لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِىَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِىٓ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kaka yangu Harun ni fasaha zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume pamoja nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi ninahofu watanikadhibisha."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَٰنًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا بِـَٔايَٰتِنَآ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلْغَٰلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema, "Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na tutawapa mamlaka, kwa hivyo hawatawafikilia. Kwa sababu ya Ishara zetu, nyinyi na watakaowafuata ndio mtashinda."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَهُم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا بَيِّنَٰتٍ قَالُوا۟ مَا هَٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِىٓ ءَابَآئِنَا ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Musa alipowafikia na Ishara zetu, walisema, "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi uliozuliwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّىٓ أَعْلَمُ بِمَن جَآءَ بِٱلْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِۦ وَمَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa akasema, "Mola wangu Mlezi ni Mwenye kujua kabisa ni nani anayekuja na uongofu unaotoka kwake, na ni nani atakayekuwa na mwisho mwema wa makazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرِى فَأَوْقِدْ لِى يَٰهَٰمَٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجْعَل لِّى صَرْحًا لَّعَلِّىٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّى لَأَظُنُّهُۥ مِنَ ٱلْكَٰذِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Firauni akasema, "Enyi waheshimiwa, sijawahi kujua kama mnaye mungu asiyekuwa mimi. Ewe Haman, niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi ninamwona yeye ni katika waongo."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُۥ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kuwa hawatarudishwa kwetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخَذْنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَٰهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى ٱلنَّارِ وَيَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ لَا يُنصَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَتْبَعْنَٰهُمْ فِى هَٰذِهِ ٱلدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ هُم مِّنَ ٱلْمَقْبُوحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanaochusha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَٰبَ مِنۢ بَعْدِ مَآ أَهْلَكْنَا ٱلْقُرُونَ ٱلْأُولَىٰ بَصَآئِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha kuziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلْغَرْبِىِّ إِذْ قَضَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَى ٱلْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ ٱلشَّٰهِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri, wala hukuwa katika waliohudhuria.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَٰكِنَّآ أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِىٓ أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتِنَا وَلَٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkazi na watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tuliokuwa tukiwatuma Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hukuwa kando ya mlima ule tuliponadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiopata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْلَآ أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌۢ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا۟ رَبَّنَا لَوْلَآ أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ وَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa usije kuwasibu msiba kwa iliyoyatanguliza mikono yao, wakasema, "Ewe Mola wetu Mlezi, mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa miongoni mwa Waumini?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا۟ لَوْلَآ أُوتِىَ مِثْلَ مَآ أُوتِىَ مُوسَىٰٓ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا۟ بِمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ قَالُوا۟ سِحْرَانِ تَظَٰهَرَا وَقَالُوٓا۟ إِنَّا بِكُلٍّ كَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIlipowajia Haki kutoka kwetu, walisema, "Mbona hakupewa kama aliyopewa Musa?" Je, kwani wao hawakuyakataa aliyopewa Musa zamani? Walisema, "Ni wachawi wawili wanasaidiana." Na wakasema, "Hakika sisi tunawakataa wote."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ فَأْتُوا۟ بِكِتَٰبٍ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَآ أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Basi leteni Kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kilicho kiongofu zaidi kuliko hivi viwili nikifuate, kama nyinyi ni wakweli."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَكَ فَٱعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَآءَهُمْ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu. Na ni nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata matamanio yake bila ya uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ ٱلْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sasa kwa yakini tumewafikishia Neno moja baada ya lingine ili wapate kukumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَٰهُمُ ٱلْكِتَٰبَ مِن قَبْلِهِۦ هُم بِهِۦ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale tuliowapa Kitabu kabla yake wanakiamini hiki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِۦ مُسْلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa, wanasema, "Tunaiamini. Hakika hii ndiyo Haki inayotoka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulionyenyekea."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا۟ وَيَدْرَءُونَ بِٱلْحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَٰهُمْ يُنفِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao watapewa ujira wao mara mbili kwa walivyovumilia, na wakaondoa ubaya kwa wema, na wakatoa katika tulivyowaruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا سَمِعُوا۟ ٱللَّغْوَ أَعْرَضُوا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ لَنَآ أَعْمَٰلُنَا وَلَكُمْ أَعْمَٰلُكُمْ سَلَٰمٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِى ٱلْجَٰهِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposikia upuuzi, hujitenga nao na husema, "Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum (Amani iwe juu yenu)! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّكَ لَا تَهْدِى مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يَشَآءُ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika, wewe humwongoi umpendaye. Lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوٓا۟ إِن نَّتَّبِعِ ٱلْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَآ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا ءَامِنًا يُجْبَىٰٓ إِلَيْهِ ثَمَرَٰتُ كُلِّ شَىْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema, "Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe, tutanyakuliwa kutoka nchi yetu." Je, kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍۭ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا فَتِلْكَ مَسَٰكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّنۢ بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا وَكُنَّا نَحْنُ ٱلْوَٰرِثِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miji mingapi iliyojifahirisha katika maisha yao tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao, isipokuwa kwa uchache tu. Na Sisi ndio tumekuwa warithi wao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ ٱلْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِىٓ أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتِنَا وَمَا كُنَّا مُهْلِكِى ٱلْقُرَىٰٓ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَٰلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَىْءٍ فَمَتَٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَزِينَتُهَا وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa chochote mlichopewa, ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na yatakayobaki zaidi. Basi je, hamfahamu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَن وَعَدْنَٰهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَٰهُ مَتَٰعَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, yule tuliyemuahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَغْوَيْنَآ أَغْوَيْنَٰهُمْ كَمَا غَوَيْنَا تَبَرَّأْنَآ إِلَيْكَ مَا كَانُوٓا۟ إِيَّانَا يَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema wale iliyothibiti juu yao kauli, "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِيلَ ٱدْعُوا۟ شُرَكَآءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُمْ وَرَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ يَهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa itasemwa, "Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu!" Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَآ أَجَبْتُمُ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakapowaita na akasema, "Mliwajibu nini Mitume?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْأَنۢبَآءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَآءَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi zitawapotea habari siku hiyo, nao hawataulizana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحًا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلْمُفْلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufaulu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخْتَارُ مَا كَانَ لَهُمُ ٱلْخِيَرَةُ سُبْحَٰنَ ٱللَّهِ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi huumba na huteua atakavyo. Viumbe hawana hiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi anayajua viliyoyaficha vifua vyao, na wanayoyaweka hadharani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ لَهُ ٱلْحَمْدُ فِى ٱلْأُولَىٰ وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَلَهُ ٱلْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمُ ٱلَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَٰمَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ يَأْتِيكُم بِضِيَآءٍ أَفَلَا تَسْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea mwangaza? Basi je, hamsikii?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمُ ٱلنَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَٰمَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ أَفَلَا تُبْصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya mchana umewakalia moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atayewaletea usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِن رَّحْمَتِهِۦ جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni katika rehema zake amewafanyia usiku na mchana ili mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi hao mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا۟ بُرْهَٰنَكُمْ فَعَلِمُوٓا۟ أَنَّ ٱلْحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema, "Leteni hoja zenu!" Hapo watajua kwamba hakika haki ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ قَٰرُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ وَءَاتَيْنَٰهُ مِنَ ٱلْكُنُوزِ مَآ إِنَّ مَفَاتِحَهُۥ لَتَنُوٓأُ بِٱلْعُصْبَةِ أُو۟لِى ٱلْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُۥ قَوْمُهُۥ لَا تَفْرَحْ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْفَرِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhuluma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzibeba. Watu wake walipomwambia, "Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱبْتَغِ فِيمَآ ءَاتَىٰكَ ٱللَّهُ ٱلدَّارَ ٱلْـَٔاخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ ٱلدُّنْيَا وَأَحْسِن كَمَآ أَحْسَنَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ ٱلْفَسَادَ فِى ٱلْأَرْضِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُفْسِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu, makazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la duniani. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya uharibifu katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao uharibifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِىٓ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِۦ مِنَ ٱلْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا وَلَا يُسْـَٔلُ عَن ذُنُوبِهِمُ ٱلْمُجْرِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo." Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wahalifu hawataulizwa habari ya dhambi zao."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِۦ فِى زِينَتِهِۦ قَالَ ٱلَّذِينَ يُرِيدُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا يَٰلَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَآ أُوتِىَ قَٰرُونُ إِنَّهُۥ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani, "Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ ٱللَّهِ خَيْرٌ لِّمَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحًا وَلَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلصَّٰبِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema wale waliopewa elimu, "Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipokuwa wenye subira."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَخَسَفْنَا بِهِۦ وَبِدَارِهِ ٱلْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُۥ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُنتَصِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kando na Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَصْبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوْا۟ مَكَانَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ لَوْلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا وَيْكَأَنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliotamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema, "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye. Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani, angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi!"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تِلْكَ ٱلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا وَٱلْعَٰقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujiinua juu katika dunia wala uharibifu. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَن جَآءَ بِٱلْحَسَنَةِ فَلَهُۥ خَيْرٌ مِّنْهَا وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى ٱلَّذِينَ عَمِلُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ إِلَّا مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtakayetenda mazuri, atapata malipo bora kuliko hayo mazuri aliyoyatenda. Na atakayetenda mabaya, hawalipwi watendao mabaya isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِى فَرَضَ عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ مَن جَآءَ بِٱلْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yule aliyekulazimisha kuifuata Qur-ani, hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema, "Mola wangu Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uongofu, na ni nani aliyemo katika upotovu ulio dhahiri."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كُنتَ تَرْجُوٓا۟ أَن يُلْقَىٰٓ إِلَيْكَ ٱلْكِتَٰبُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawe hukuwa unataraji kuletewa Kitabu; lakini ni rehema tu ya Mola wako Mlezi. Basi kamwe usiwe msaidizi wa makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ وَٱدْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala kamwe wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na lingania kwa Mola wako Mlezi, wala kamwe usiwe miongoni mwa washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ كُلُّ شَىْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُۥ لَهُ ٱلْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwinginewe. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake. Hukumu ni yake, na kwake mtarejeshwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70