caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Naml, Aya 44

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 48 · 27:44

قِيلَ لَهَا ٱدْخُلِى ٱلصَّرْحَ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا قَالَ إِنَّهُۥ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipoliona, alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Suleiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lililofanyiwa sakafu ya vioo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu, na sasa ninanyenyekea pamoja na Suleiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAkaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70