أَمَّن يُجِيبُ ٱلْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ ٱلسُّوٓءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَآءَ ٱلْأَرْضِ أَءِلَٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani yule anayemjibu mwenye shida kubwa pale anapomwomba, na akaiondoa dhiki, na akawafanya warithi wa ardhi? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayoyazingatia.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAu nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.