فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَٰذَا رَبِّى هَٰذَآ أَكْبَرُ فَلَمَّآ أَفَلَتْ قَالَ يَٰقَوْمِ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipoliona jua linachomoza, akasema: 'Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi.' Na lilipotua, akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali sana na hayo mnayoshirikisha.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina.