وَإِذَا رَأَيْتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِىٓ ءَايَٰتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا۟ فِى حَدِيثٍ غَيْرِهِۦ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيْطَٰنُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ ٱلذِّكْرَىٰ مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unapowaona wanaoziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shetani atakusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhalimu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu.