caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 124

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:124

وَإِذَا جَآءَتْهُمْ ءَايَةٌ قَالُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَآ أُوتِىَ رُسُلُ ٱللَّهِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُۥ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَمْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa inapowajia Ishara, wao husema: 'Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu.' Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu, na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70