caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 70

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:70

وَذَرِ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَذَكِّرْ بِهِۦٓ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌۢ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِىٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَآ أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أُبْسِلُوا۟ بِمَا كَسَبُوا۟ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaachilie mbali walioifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawadanganya. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyoyachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingetoa kila fidia, haitokubaliwa. Hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyokuwa wakikufuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWaachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70