caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 6

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:6

أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا ٱلْأَنْهَٰرَ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَٰهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِنۢ بَعْدِهِمْ قَرْنًا ءَاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao? Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha nyinyi; na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao. Mwishowe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJee, hawaoni vizazi vingapi tulivyo viangamiza kabla yao? Tuliwaweka katika nchi tusivyo kuwekeni nyinyi; tukawapelekea mvua nyingi na tukaifanya mito inapita chini yao. Mwishoe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70