سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشْرَكْنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَىْءٍ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا۟ بَأْسَنَا قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَآ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema wale walioshirikisha, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, tusingelishirikisha, wala baba zetu, wala tusingeliharamisha kitu chochote." Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao mpaka walipoionja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo? Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu.