وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِن يَرَوْا۟ كُلَّ ءَايَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا۟ بِهَا حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوكَ يُجَٰدِلُونَكَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza; na tumezitia pazia kwenye nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi katika masikio yao, na wakiona kila Ishara, hawaiamini. Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si chochote ila hadithi za watu wa kale.