caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 125

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:125

فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهْدِيَهُۥ يَشْرَحْ صَدْرَهُۥ لِلْإِسْلَٰمِ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُۥ يَجْعَلْ صَدْرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِى ٱلسَّمَآءِ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumuongoa, humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule anayetaka kumpoteza, hukifanya kifua chake kuwa na dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda katika mbingu kwa ugumu mkubwa. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anaweka uchafu juu ya wale wasioamini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70