قُلْ إِنَّنِى هَدَىٰنِى رَبِّىٓ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Hakika mimi, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye njia iliyonyooka, dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahim aliyekuwa mnyofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.