caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 151

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:151

قُلْ تَعَالَوْا۟ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلَّا تُشْرِكُوا۟ بِهِۦ شَيْـًٔا وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَٰنًا وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَوْلَٰدَكُم مِّنْ إِمْلَٰقٍ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ وَلَا تَقْرَبُوا۟ ٱلْفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَلَا تَقْتُلُوا۟ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Njooni niwasomee yale aliyowaharamishia Mola wenu Mlezi: Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote, na wazazi wawili wafanyieni uzuri, wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao. Wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake. Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharamisha isipokuwa kwa haki. Hayo aliwausia ili myatie akilini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70