وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ قَدِ ٱسْتَكْثَرْتُم مِّنَ ٱلْإِنسِ وَقَالَ أَوْلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلْإِنسِ رَبَّنَا ٱسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِىٓ أَجَّلْتَ لَنَا قَالَ ٱلنَّارُ مَثْوَىٰكُمْ خَٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ile Siku atakapowakusanya wote, “Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu.” Na marafiki zao katika wanadamu watasema: 'Mola wetu Mlezi! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu, na tumefikia muda wetu uliotuwekea.' Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndiyo makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mwenye kujua zaidi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua.