قُلْ أَنَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِى ٱسْتَهْوَتْهُ ٱلشَّيَٰطِينُ فِى ٱلْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُۥٓ أَصْحَٰبٌ يَدْعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلْهُدَى ٱئْتِنَا قُلْ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلْهُدَىٰ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa? Tuwe kama ambao mashetani wamempumbaza katika ardhi, amechanganyikiwa? Anao marafiki wanaomwita aende kwenye uwongofu, wakimwambia: 'Njoo kwetu!' Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote,