ثَمَٰنِيَةَ أَزْوَٰجٍ مِّنَ ٱلضَّأْنِ ٱثْنَيْنِ وَمِنَ ٱلْمَعْزِ ٱثْنَيْنِ قُلْ ءَآلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلْأُنثَيَيْنِ أَمَّا ٱشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ ٱلْأُنثَيَيْنِ نَبِّـُٔونِى بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Amewaumbia) majozi manane: katika kondoo ni wawili, na katika mbuzi ni wawili. Sema: Je, ameharamisha madume wawili hawa au majike wawili hawa, au wale walio matumboni mwa majike yote mawili haya? Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAmekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.