caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-An'aam, Aya 158

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 55 · 6:158

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِىَ بَعْضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ يَوْمَ يَأْتِى بَعْضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَٰنُهَا لَمْ تَكُنْ ءَامَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِىٓ إِيمَٰنِهَا خَيْرًا قُلِ ٱنتَظِرُوٓا۟ إِنَّا مُنتَظِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanangoja isipokuwa kwamba wajiwe na Malaika, au awajie Mola wako Mlezi, au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake. Sema, "Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70