وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَكُمْ خَلَٰٓئِفَ ٱلْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَٰتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِى مَآ ءَاتَىٰكُمْ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلْعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌۢ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyewafanya kuwa wafuatizi (makhalifa) katika ardhi, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali ili akujaribuni katika hayo aliyowapa. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNaye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.