وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا كُلَّ ذِى ظُفُرٍ وَمِنَ ٱلْبَقَرِ وَٱلْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلْحَوَايَآ أَوْ مَا ٱخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ذَٰلِكَ جَزَيْنَٰهُم بِبَغْيِهِمْ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mayahudi tuliwaharamishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko. Na katika ng'ombe, na kondoo, na mbuzi tuliwaharamishia shahamu yao, isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao, au iliyochanganyika na mifupa. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao. Nasi bila ya shaka ni wakweli.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.