وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا۟ مِمَّا ذُكِرَ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا ٱضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَآئِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُعْتَدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mna nini msile katika vile vilivyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwishawabainishia kwa kina vile alivyowaharamishia, isipokuwa vile mnavyolazimishwa? Na hakika wengi wanapotea kwa matamanio yao bila ya kuwa na elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua vyema wale wanaopindukia mipaka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kwa nini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka.