أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْتَغِى حَكَمًا وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ إِلَيْكُمُ ٱلْكِتَٰبَ مُفَصَّلًا وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَٰهُمُ ٱلْكِتَٰبَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِٱلْحَقِّ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina? Na wale tuliowapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi kamwe usiwe katika wale wanaotia shaka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.