Mwanzo › Sura › Sura At-Tur
Sura At-Tur الطور
Aya 49 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 76
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلطُّورِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa mlima wa T'ur.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكِتَٰبٍ مَّسْطُورٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Kitabu kilichoandikwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فِى رَقٍّ مَّنشُورٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Katika ngozi iliyokunjuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْبَيْتِ ٱلْمَعْمُورِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa Nyumba iliyojengwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلسَّقْفِ ٱلْمَرْفُوعِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa dari iliyonyanyuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْبَحْرِ ٱلْمَسْجُورِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa bahari iliyojazwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hapana wa kuizuia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوْرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku zitakapotikisika mbingu kwa mtikiso.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَسِيرُ ٱلْجِبَالُ سَيْرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ هُمْ فِى خَوْضٍ يَلْعَبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukadhibisha!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَسِحْرٌ هَٰذَآ أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, huu ni uchawi, au hamwoni tu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱصْلَوْهَا فَٱصْبِرُوٓا۟ أَوْ لَا تَصْبِرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْكُمْ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyokuwa mkiyatenda.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّٰتٍ وَنَعِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na neema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakifurahi kwa yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda kutokana na adhabu ya Motoni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ وَزَوَّجْنَٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyopangwa kwa safu. Na tutawaoza mahurulaini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَآ أَلَتْنَٰهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَىْءٍ كُلُّ ٱمْرِئٍۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wale walioamini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani, tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alichokichuma.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَمْدَدْنَٰهُم بِفَٰكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tutawapa matunda, na nyama kama watakavyopenda.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Watapeana humo bilauri zisizo na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wataelekeana wakiulizana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِىٓ أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Waseme: Hakika tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa mno.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda mbali adhabu ya upepo wa Moto.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْبَرُّ ٱلرَّحِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwingi wa kurehemu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيْبَ ٱلْمَنُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ تَرَبَّصُوا۟ فَإِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُتَرَبِّصِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَٰمُهُم بِهَٰذَآ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au ndiyo wanasema: 'Ameitunga hii!' Bali basi tu hawaamini!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلْيَأْتُوا۟ بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِۦٓ إِن كَانُوا۟ صَٰدِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ خُلِقُوا۟ مِنْ غَيْرِ شَىْءٍ أَمْ هُمُ ٱلْخَٰلِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ خَلَقُوا۟ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بَل لَّا يُوقِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ ٱلْمُصَۣيْطِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanazo hazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَٰنٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja iliyo wazi!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَهُ ٱلْبَنَٰتُ وَلَكُمُ ٱلْبَنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanayo elimu ya ghaibu, nao wameandika?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هُمُ ٱلْمَكِيدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao waliokufuru ndio watakaotegeka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَهُمْ إِلَٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ سُبْحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanaye mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ametakasika Mwenyezi Mungu mbali na hao wanaowashirikisha naye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِن يَرَوْا۟ كِسْفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطًا يَقُولُوا۟ سَحَابٌ مَّرْكُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hata wangeona pande linatoka mbinguni linaanguka wangesema: Ni mawingu yaliyobebana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى فِيهِ يُصْعَقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapohilikishwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ لَا يُغْنِى عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hii, lakini wengi wao hawajui.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَٰرَ ٱلنُّجُومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Adh-Dhaariyat
Sura An-Najm →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.