Mwanzo › Sura › Sura Adh-Dhaariyat
Sura Adh-Dhaariyat الذاريات
Aya 60 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 67
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرْوًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa pepo zinazotawanya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱلْحَٰمِلَٰتِ وِقْرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na zinazobeba mizigo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱلْجَٰرِيَٰتِ يُسْرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na zinazokwenda kwa wepesi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱلْمُقَسِّمَٰتِ أَمْرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na zinazogawanya kwa amri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni ya ukweli.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْحُبُكِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa mbingu zenye njia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّكُمْ لَفِى قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayohitalifiana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُتِلَ ٱلْخَرَّٰصُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wazushi wameangamizwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ هُمْ فِى غَمْرَةٍ سَاهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao wameghafilika katika ujinga.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَسْـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلدِّينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanauliza: 'Ni lini hiyo siku ya malipo?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ هُمْ عَلَى ٱلنَّارِ يُفْتَنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ذُوقُوا۟ فِتْنَتَكُمْ هَٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyokuwa mkiyafanyia haraka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani ya mbinguni na chemchemi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanapokea yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَانُوا۟ قَلِيلًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَبِٱلْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِى ٱلْأَرْضِ ءَايَٰتٌ لِّلْمُوقِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِىٓ أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na pia katika nafsi zenu - Je, hamwoni?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika mbingu ziko riziki zenu na yale mnayoahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَآ أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ninaapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْمُكْرَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaoheshimiwa?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَٰمًا قَالَ سَلَٰمٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Walipoingia kwake na wakasema: 'Salama!' Na yeye akasema: 'Salama! Nyinyi ni watu nisiowajua.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi akaenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akawakaribishia, akasema: 'Mbona hamli?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً قَالُوا۟ لَا تَخَفْ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: 'Usiwe na hofu.' Basi wakambashiria kupata kijana mwenye elimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَقْبَلَتِ ٱمْرَأَتُهُۥ فِى صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ndipo mkewe akawaelekea kwa sauti ya kelele huku anajipiga usoni kwa mastaajabu, akasema: "Mimi ni kikongwe na tasa!"
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: 'Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: 'Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Tuwatupie mawe ya udongo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hivyo tukawatoa katika hao wale walioamini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ ٱلْمُسْلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَرَكْنَا فِيهَآ ءَايَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِى مُوسَىٰٓ إِذْ أَرْسَلْنَٰهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَٰنٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika habari za Musa, tulipomtuma kwa Firauni na hoja wazi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu!'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَخَذْنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, huku ni wa kulaumiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِى عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلْعَقِيمَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika habari za 'Adi tulipowatumia upepo wa kukata uzazi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا تَذَرُ مِن شَىْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَٱلرَّمِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichonyambuka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِى ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا۟ حَتَّىٰ حِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika habari za Thamudi walipoambiwa: 'Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَعَتَوْا۟ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi ukawanyakua moto wa radi nao wanaona.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا ٱسْتَطَٰعُوا۟ مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا۟ مُنتَصِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَٰسِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَٰهَا بِأَيْي۟دٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْأَرْضَ فَرَشْنَٰهَا فَنِعْمَ ٱلْمَٰهِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِن كُلِّ شَىْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَفِرُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا تَجْعَلُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا۟ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَتَوَاصَوْا۟ بِهِۦ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَذَكِّرْ فَإِنَّ ٱلذِّكْرَىٰ تَنفَعُ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا خَلَقْتُ ٱلْجِنَّ وَٱلْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَآ أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلْقُوَّةِ ٱلْمَتِينُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَٰبِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wale waliodhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasiniharakishe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن يَوْمِهِمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ole wao wale walioikanusha siku yao waliyoahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Qaaf
Sura At-Tur →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.