Mwanzo › Sura › Sura Al-Qalam
Sura Al-Qalam القلم
Aya 52 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 2
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ نٓ وَٱلْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nuun. Ninaapa kwa kalamu na yale wayaandikayo.[1]
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَآ أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika wewe una tabia tukufu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Karibu utaona, na wao wataona.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بِأَييِّكُمُ ٱلْمَفْتُونُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Mola wako Mlezi ndiye ajuaye zaidi ni nani aliyeipotea njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَا تُطِعِ ٱلْمُكَذِّبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi usiwatii wanaokadhibisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَدُّوا۟ لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Walitamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala usimtii kila mwingi wa kuapa, anayedharauliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَمَّازٍ مَّشَّآءٍۭ بِنَمِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwenye kukejeli mno, anayetangatanga akieneza maneno ya kufitini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwenye kuzuia mno heri, dhalimu, mwingi wa madhambi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عُتُلٍّۭ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mkatili, na juu ya hayo, ni mshari aliyejipachika tu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ati kwa kuwa ana mali na watoto!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Anaposomewa Aya zetu, husema: "(Hizi ni) simulizi za uongo za watu wa zamani!"
Tazama tafsiri zote za aya hii →
سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلْخُرْطُومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Tutamtia alama kwenye pua yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا بَلَوْنَٰهُمْ كَمَا بَلَوْنَآ أَصْحَٰبَ ٱلْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا۟ لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika tuliwajaribu hawa kama tulivyowajaribu wale wenye shamba, walipoapa kwamba lazima watayavuna mazao yake itakapokuwa asubuhi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا يَسْتَثْنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hawakusema: "Mwenyezi Mungu akipenda!"
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَطَافَ عَلَيْهَا طَآئِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَآئِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَصْبَحَتْ كَٱلصَّرِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Likawa kama usiku wa giza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَتَنَادَوْا۟ مُصْبِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha asubuhi wakaitana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَنِ ٱغْدُوا۟ عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَٰرِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ya kwamba: "Nendeni mapema kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna."
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱنطَلَقُوا۟ وَهُمْ يَتَخَٰفَتُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi walikwenda huku wananong'onezana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا ٱلْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ya kuwa: "Leo kamwe masikini mmoja asikuingilieni."
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَغَدَوْا۟ عَلَىٰ حَرْدٍ قَٰدِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوٓا۟ إِنَّا لَضَآلُّونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali tumenyimwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ سُبْحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَٰوَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi wakaelekeana kulaumiana wao kwa wao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ يَٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa tumeikiuka mipaka!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَذَٰلِكَ ٱلْعَذَابُ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangelijua!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wacha Mungu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَنَجْعَلُ ٱلْمُسْلِمِينَ كَٱلْمُجْرِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani tutawafanya Waislamu kama wahalifu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mna nini? Mnahukumu vipi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَكُمْ كِتَٰبٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kuwa mtapata humo mnayoyapenda?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَكُمْ أَيْمَٰنٌ عَلَيْنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayojihukumia?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa haya?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَهُمْ شُرَكَآءُ فَلْيَأْتُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ إِن كَانُوا۟ صَٰدِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza
Tazama tafsiri zote za aya hii →
خَٰشِعَةً أَبْصَٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ وَقَدْ كَانُوا۟ يُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمْ سَٰلِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipokuwa wazima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَرْنِى وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلْحَدِيثِ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi niache na wanaokadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kutokea mahali wasipopajua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأُمْلِى لَهُمْ إِنَّ كَيْدِى مَتِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, aliponadi naye kazongwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّوْلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angelitupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱجْتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَٰرِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا۟ ٱلذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجْنُونٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Mulk
Sura Al-Haaqqa →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.