caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Mulk الملك

Aya 30 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 77

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ تَبَٰرَكَ ٱلَّذِى بِيَدِهِ ٱلْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْمَوْتَ وَٱلْحَيَوٰةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْغَفُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye msamaha mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَٰوَٰتٍ طِبَاقًا مَّا تَرَىٰ فِى خَلْقِ ٱلرَّحْمَٰنِ مِن تَفَٰوُتٍ فَٱرْجِعِ ٱلْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudia kutazama! Je, unaona kosa lolote?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ ٱرْجِعِ ٱلْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ ٱلْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTena rudia kutazama mara mbili, kutazama kwako kutakurejelea mwenyewe hali ya kuwa kumehizika, kumechoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِمَصَٰبِيحَ وَجَعَلْنَٰهَا رُجُومًا لِّلشَّيَٰطِينِ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa hakika tumeipamba mbingu ya chini kabisa kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto wenye mwako mkali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذَآ أُلْقُوا۟ فِيهَا سَمِعُوا۟ لَهَا شَهِيقًا وَهِىَ تَفُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatakapotupwa humo, watausikia mngurumo wake na huku inafoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلْغَيْظِ كُلَّمَآ أُلْقِىَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَآ أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterInakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo, walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَلَىٰ قَدْ جَآءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَٰلٍ كَبِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!''

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِىٓ أَصْحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watasema: 'Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!'

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱعْتَرَفُوا۟ بِذَنۢبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Moto wenye mwako mkali!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu, watapata maghfira na ujira mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَسِرُّوا۟ قَوْلَكُمْ أَوِ ٱجْهَرُوا۟ بِهِۦٓ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi; hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلْخَبِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAsijue yule aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ ذَلُولًا فَٱمْشُوا۟ فِى مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا۟ مِن رِّزْقِهِۦ وَإِلَيْهِ ٱلنُّشُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndiyo kufufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ءَأَمِنتُم مَّن فِى ٱلسَّمَآءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ ٱلْأَرْضَ فَإِذَا هِىَ تَمُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mmesalimika kutokana na aliyeko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِى ٱلسَّمَآءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَٰٓفَّٰتٍ وَيَقْبِضْنَ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا ٱلرَّحْمَٰنُ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَىْءٍۭ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyozikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona mno kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمَّنْ هَٰذَا ٱلَّذِى هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ ٱلرَّحْمَٰنِ إِنِ ٱلْكَٰفِرُونَ إِلَّا فِى غُرُورٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema? Hakika makafiri hawamo ila katika udanganyifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمَّنْ هَٰذَا ٱلَّذِى يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُۥ بَل لَّجُّوا۟ فِى عُتُوٍّ وَنُفُورٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na kujiweka mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَن يَمْشِى مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِۦٓ أَهْدَىٰٓ أَمَّن يَمْشِى سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia iliyonyooka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Yeye ndiye aliyekuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni uwezo wa kusikia na kuona na ufahamu wa nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هُوَ ٱلَّذِى ذَرَأَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Yeye ndiye aliyekutawanyeni katika ardhi, na kwake mtakusanywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema ukweli?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّمَا ٱلْعِلْمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu; na hakika mimi ni mwonyaji wa wazi tu mwenye kubainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيٓـَٔتْ وُجُوهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَقِيلَ هَٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَدَّعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini watakapoiona karibu, nyuso za wale waliokufuru zitahuzunishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِىَ ٱللَّهُ وَمَن مَّعِىَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ ٱلْكَٰفِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na wale walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakayewalinda makafiri mbali na adhabu chungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هُوَ ٱلرَّحْمَٰنُ ءَامَنَّا بِهِۦ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Basi mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَآؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَآءٍ مَّعِينٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, ni nani atakuleteeni maji yanayomiminika?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70