Mwanzo › Sura › Sura Qaaf
Sura Qaaf ق
Aya 45 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 34
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ قٓ وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْمَجِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Qaaf.[1] Ninaapa kwa Qur-ani tukufu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ عَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ ٱلْكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَىْءٌ عَجِيبٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: 'Hili ni jambo la ajabu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ذَٰلِكَ رَجْعٌۢ بَعِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ ٱلْأَرْضُ مِنْهُمْ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظٌۢ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi vyema yote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ كَذَّبُوا۟ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ فَهُمْ فِىٓ أَمْرٍ مَّرِيجٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini waliikanusha Haki ilipowajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mchanganyiko.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَلَمْ يَنظُرُوٓا۟ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَٰهَا وَزَيَّنَّٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyozijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْأَرْضَ مَدَدْنَٰهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍۭ بَهِيجٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kurejea (kwa Mwenyezi Mungu).
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَزَّلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً مُّبَٰرَكًا فَأَنۢبَتْنَا بِهِۦ جَنَّٰتٍ وَحَبَّ ٱلْحَصِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلنَّخْلَ بَاسِقَٰتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mitende mirefu yenye makole yaliyozaa kwa wingi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ وَأَحْيَيْنَا بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا كَذَٰلِكَ ٱلْخُرُوجُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakazi wa Rassi na Thamudi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَٰنُ لُوطٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na A'di na Firauni na kaumu ya Luti.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَصْحَٰبُ ٱلْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ كُلٌّ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wakazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَعَيِينَا بِٱلْخَلْقِ ٱلْأَوَّلِ بَلْ هُمْ فِى لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza? Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَٰنَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِۦ نَفْسُهُۥ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ ٱلْوَرِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tulimuumba mtu, nasi tunayajua yanayomtia wasiwasi katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذْ يَتَلَقَّى ٱلْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanapopokea wapokeaji wawili, wanaokaa kuliani na kushotoni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَآءَتْ سَكْرَةُ ٱلْمَوْتِ بِٱلْحَقِّ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyokuwa ukiyakimbia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْوَعِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَآءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَآئِقٌ وَشَهِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّقَدْ كُنتَ فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلْيَوْمَ حَدِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Aambiwe): 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya. Basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَٰذَا مَا لَدَىَّ عَتِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mwenzake atasema: 'Huyu niliye naye mimi keshatayarishwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَلْقِيَا فِى جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mtupeni katika Jahanamu kila kafiri mkubwa mkaidi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akatazaye mno heri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِى جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Aliyeweka mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطْغَيْتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِى ضَلَٰلٍۭ بَعِيدٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwenzake aseme: 'Ewe Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا۟ لَدَىَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِٱلْوَعِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Mwenyezi Mungu) aseme: 'Msigombane mbele yangu. Tayari niliwaletea mbele onyo langu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا يُبَدَّلُ ٱلْقَوْلُ لَدَىَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّٰمٍ لِّلْعَبِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku tutakapoiambia Jahanamu: 'Je, umejaa?' Nayo itasema: 'Je, kuna ziada?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأُزْلِفَتِ ٱلْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Bustani ya mbinguni italetwa karibu mno kwa ajili ya wacha Mungu, haitakuwa mbali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Haya ndiyo mnayoahidiwa kwa kila mwenye kurejea mno kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda vyema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَّنْ خَشِىَ ٱلرَّحْمَٰنَ بِٱلْغَيْبِ وَجَآءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwenye kumwogopa mno Mwingi wa rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo uliotubia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱدْخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْخُلُودِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Ataambiwa) ingieni humo kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya kudumu daima dawamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا۟ فِى ٱلْبِلَٰدِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, waliokuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je, walipata pa kukimbilia?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى ٱلسَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita; na wala hayakutugusa machovu yoyote.[1]
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ ٱلشَّمْسِ وَقَبْلَ ٱلْغُرُوبِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَٰرَ ٱلسُّجُودِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ ٱلْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na sikiliza siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka mahali karibu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ يَسْمَعُونَ ٱلصَّيْحَةَ بِٱلْحَقِّ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْخُرُوجِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku watakaposikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا نَحْنُ نُحْىِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا ٱلْمَصِيرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ تَشَقَّقُ ٱلْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ فَذَكِّرْ بِٱلْقُرْءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeliogopa onyo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Hujuraat
Sura Adh-Dhaariyat →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.