caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Kahf, Aya 49

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 69 · 18:49

وَوُضِعَ ٱلْكِتَٰبُ فَتَرَى ٱلْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَٰوَيْلَتَنَا مَالِ هَٰذَا ٱلْكِتَٰبِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّآ أَحْصَىٰهَا وَوَجَدُوا۟ مَا عَمِلُوا۟ حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kitawekwa mbele Kitabu. Basi utawaona wahalifu wanavyoogopa mno kwa sababu ya yale yaliyomo. Na watasema: "Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kililidhibiti vyema?" Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70