وَقُلِ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَآءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَآءَ فَلْيَكْفُرْ إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلظَّٰلِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا وَإِن يَسْتَغِيثُوا۟ يُغَاثُوا۟ بِمَآءٍ كَٱلْمُهْلِ يَشْوِى ٱلْوُجُوهَ بِئْسَ ٱلشَّرَابُ وَسَآءَتْ مُرْتَفَقًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akufuru. Hakika Sisi tumewaandalia madhalimu Moto ambao kuta zake zitawazingira. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji yaliyo kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilichoje hicho, na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia palipoje hapo!
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama khema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!