وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِىَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى ٱلْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeziba nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi uko kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uongofu, kamwe hawataweza kuongoka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ni nani dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyo tangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uwongofu hawakubali kabisa kuongoka.