caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Kahf, Aya 22

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 69 · 18:22

سَيَقُولُونَ ثَلَٰثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًۢا بِٱلْغَيْبِ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَآءً ظَٰهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.ˮ Wanabahatisha ghaibu. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: “Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Hawawajui isipokuwa wachache tu.ˮ Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule miongoni mwao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70