Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa ucha Mungu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau wao wangelingojea mpaka uwatokee, ingelikuwa heri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Akikujieni mpotovu na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amewafanya muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi, basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane heshima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba mno, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye habari.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMabedui walisema: 'Tumeamini.' Sema: 'Hamjaamini, lakini semeni: 'Tumesilimu.' Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Waumini ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: 'Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kitu?'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: 'Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.'