Sura Al-Mutaffifin المطففين
Aya 36 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 86
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterOle wao hao wapunjao!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكْتَالُوا۟ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسْتَوْفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَلَا يَظُنُّ أُو۟لَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِيَوْمٍ عَظِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika Siku iliyo kuu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلْفُجَّارِ لَفِى سِجِّينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سِجِّينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterUnajua nini Sijjin?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كِتَٰبٌ مَّرْقُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKitabu kilichoandikwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterOle wao siku hiyo kwa wanaokadhibisha!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnaposomewa Aya zetu husema: "Ni visa vya watu wa kale!"
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا بَلْ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa mbali na neema za Mola wao Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُوا۟ ٱلْجَحِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha wataingia Motoni!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha waambiwe: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhibisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلْأَبْرَارِ لَفِى عِلِّيِّينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika Illiyyin.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa nini kitakachokujuvya nini Iliyyin?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كِتَٰبٌ مَّرْقُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKitabu kilichoandikwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَشْهَدُهُ ٱلْمُقَرَّبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakishuhudia waliokaribishwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تَعْرِفُ فِى وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterUtatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatanyweshwa kinywaji safi kilichozibwa vyema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
خِتَٰمُهُۥ مِسْكٌ وَفِى ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ ٱلْمُتَنَٰفِسُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKizibo chake ni miski. Na katika hayo na washindanie wenye kushindana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسْنِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mchanganyiko wake ni Tasniim.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا ٱلْمُقَرَّبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterChemchemi watakayoinywa waliokurubishwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ كَانُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يَضْحَكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale waliokuwa wahalifu walikuwa wakiwacheka walioamini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا مَرُّوا۟ بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapopita karibu yao wakikonyezana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمُ ٱنقَلَبُوا۟ فَكِهِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapowaona husema: Hakika hawa ndio hasa waliopotea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أُرْسِلُوا۟ عَلَيْهِمْ حَٰفِظِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱلْيَوْمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنَ ٱلْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi leo walioamini ndio watawacheka makafiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَلْ ثُوِّبَ ٱلْكُفَّارُ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→