Mwanzo › Sura › Sura Al-Insaan
Sura Al-Insaan الانسان
Aya 31 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 98
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ هَلْ أَتَىٰ عَلَى ٱلْإِنسَٰنِ حِينٌ مِّنَ ٱلدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْـًٔا مَّذْكُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinachotajwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا خَلَقْنَا ٱلْإِنسَٰنَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَٰهُ سَمِيعًۢا بَصِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا هَدَيْنَٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلْكَٰفِرِينَ سَلَٰسِلَا۟ وَأَغْلَٰلًا وَسَعِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyochanganyika na kafuri
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni chemchemi watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُوفُونَ بِٱلنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُۥ مُسْتَطِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيُطْعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَآءً وَلَا شُكُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمِ وَلَقَّىٰهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi Mwenyezi Mungu atawalinda kutokana na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُوا۟ جَنَّةً وَحَرِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na atawalipa Bustani za mbinguni na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَٰلُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِـَٔانِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا۠
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَوَارِيرَا۟ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hiyo ni chemchemi iliyo humo inaitwa Salsabil.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasiopevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَٰلِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ وَحُلُّوٓا۟ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavishwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَآءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ تَنزِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumekuteremshia Qur-ani kidogo kidogo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ ءَاثِمًا أَوْ كَفُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرِ ٱسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَٱسْجُدْ لَهُۥ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
نَّحْنُ خَلَقْنَٰهُمْ وَشَدَدْنَآ أَسْرَهُمْ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَآ أَمْثَٰلَهُمْ تَبْدِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika haya ni mawaidha; basi anayetaka, atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu, Mwenye hekima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُدْخِلُ مَن يَشَآءُ فِى رَحْمَتِهِۦ وَٱلظَّٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًۢا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Qiyaama
Sura Al-Mursalaat →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.