Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kupishana usiku na mchana, na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyokatazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anapokijua kitu kidogo katika Aya zetu, hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuu ni uongofu. Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite merikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na ili mpate kushukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu, hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitilafiana.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanadhani wale wanaotenda maovu kuwa tutawafanya wawe sawasawa na wale walioamini, na wakatenda mema, uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya mno wanayoihukumu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe yale iliyoyachuma. Nao hawatadhulumiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu, na akaziba masikio yake, na moyo wake, na akambandika kifuniko kwenye kuona kwake? Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je, hamkumbuki?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema: 'Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuangamiza isipokuwa dahari.' Lakini wao hawana elimu ya hayo, ila wao wanadhani tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha atawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa utauona kila umma umepiga magoti, na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kuliko wazi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka, nyinyi mlikuwa mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wowote wa kuwanusuru.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote.