caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Nooh نوح

Aya 28 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 71

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ إِنَّآ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦٓ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: Kwamba waonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ يَٰقَوْمِ إِنِّى لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhahiri kwenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumtii.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi. Laiti mngejua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ إِنِّى دَعَوْتُ قَوْمِى لَيْلًا وَنَهَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَآءِىٓ إِلَّا فِرَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنِّى كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوٓا۟ أَصَٰبِعَهُمْ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَٱسْتَغْشَوْا۟ ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا۟ وَٱسْتَكْبَرُوا۟ ٱسْتِكْبَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika mimi kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنِّى دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTena niliwaita kwa uwazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنِّىٓ أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha nikawatangazia hadharani, tena nikasema nao kwa siri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقُلْتُ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُرْسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَٰلٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّٰتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَٰرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَوْا۟ كَيْفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبْعَ سَمَٰوَٰتٍ طِبَاقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلَ ٱلْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ ٱلشَّمْسَ سِرَاجًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ نَبَاتًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha atakurudisheni humo na atakutoeni tena.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ بِسَاطًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّتَسْلُكُوا۟ مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli mtembee humo katika njia zilizo pana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِى وَٱتَّبَعُوا۟ مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNuhu akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila hasara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَكَرُوا۟ مَكْرًا كُبَّارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakapanga vitimbi vikubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema: Kamwe msiiache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَدْ أَضَلُّوا۟ كَثِيرًا وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِّمَّا خَطِيٓـَٰٔتِهِمْ أُغْرِقُوا۟ فَأُدْخِلُوا۟ نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا۟ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى ٱلْأَرْضِ مِنَ ٱلْكَٰفِرِينَ دَيَّارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Nuhu akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا۟ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓا۟ إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَّبِّ ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِىَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارًۢا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70