Mwanzo › Sura › Sura Al-Ma'aarij
Sura Al-Ma'aarij المعارج
Aya 44 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 79
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ سَأَلَ سَآئِلٌۢ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِّلْكَٰفِرِينَ لَيْسَ لَهُۥ دَافِعٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مِّنَ ٱللَّهِ ذِى ٱلْمَعَارِجِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تَعْرُجُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُۥ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Malaika na Roho hupanda kwenda kwake katika siku ambayo kiasi chake ni miaka hamsini elfu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi subiri kwa subira njema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُۥ بَعِيدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wao wanaiona iko mbali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَرَىٰهُ قَرِيبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Sisi tunaiona iko karibu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلْمُهْلِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku ambayo mbingu zitakapokuwa kama madini iliyoyeyushwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na milima itakuwa kama sufi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا يَسْـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُبَصَّرُونَهُمْ يَوَدُّ ٱلْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِى مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍۭ بِبَنِيهِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ijapokuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mkewe, na nduguye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِى تُـْٔوِيهِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na jamaa zake waliokuwa wakimkimu,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّهَا لَظَىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation Center La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Unaobambua ngozi ya kichwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تَدْعُوا۟ مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰٓ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika mtu ameumbwa na papara.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Inapomgusa shari hupapatika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلْخَيْرُ مَنُوعًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na inapomgusa kheri huizuilia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا ٱلْمُصَلِّينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa wanaosali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَآئِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao wanadumisha Sala zao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ فِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba;
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuwa na amani nayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَٰفِظُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanahifadhi tupu zao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَٰنُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini wanaotaka kinyume cha haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَٰنَٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمْ قَآئِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambao wanazihifadhi Sala zao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أُو۟لَٰٓئِكَ فِى جَنَّٰتٍ مُّكْرَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hao ndio watakaoheshimiwa katika Bustani ya mbinguni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَيَطْمَعُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Bustani ya mbinguni ya neema?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّا خَلَقْنَٰهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَآ أُقْسِمُ بِرَبِّ ٱلْمَشَٰرِقِ وَٱلْمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا۟ وَيَلْعَبُوا۟ حَتَّىٰ يُلَٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayoahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
خَٰشِعَةً أَبْصَٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyokuwa wakiahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Haaqqa
Sura Nooh →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.