Mwanzo › Sura › Sura Al-Jinn
Sura Al-Jinn الجن
Aya 28 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 40
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ قُلْ أُوحِىَ إِلَىَّ أَنَّهُ ٱسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَقَالُوٓا۟ إِنَّا سَمِعْنَا قُرْءَانًا عَجَبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-ani ya ajabu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَهْدِىٓ إِلَى ٱلرُّشْدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Inaongoza kwenye uongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّهُۥ تَعَٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَٰحِبَةً وَلَا وَلَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّهُۥ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uongo uliopindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن تَقُولَ ٱلْإِنسُ وَٱلْجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uongo Mwenyezi Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ ٱلْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika walikuwako wanaume katika watu waliokuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا۟ كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ ٱللَّهُ أَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا لَمَسْنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدْنَٰهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi tulifanya bidii kufika kwenye mbingu, lakini tukazikuta zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَٰعِدَ لِلسَّمْعِ فَمَن يَسْتَمِعِ ٱلْـَٔانَ يَجِدْ لَهُۥ شِهَابًا رَّصَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا لَا نَدْرِىٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uongofu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعْجِزَ ٱللَّهَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُۥ هَرَبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا ٱلْهُدَىٰٓ ءَامَنَّا بِهِۦ فَمَن يُؤْمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi tulipousikia uongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّا مِنَّا ٱلْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا ٱلْقَٰسِطُونَ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ تَحَرَّوْا۟ رَشَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanaoacha haki. Basi waliosilimu, hao ndio waliotafuta uongofu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَمَّا ٱلْقَٰسِطُونَ فَكَانُوا۟ لِجَهَنَّمَ حَطَبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ama wanaoacha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَلَّوِ ٱسْتَقَٰمُوا۟ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَٰهُم مَّآءً غَدَقًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeliwanywesha maji kwa wingi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِۦ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anayepuuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّ ٱلْمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبْدُ ٱللَّهِ يَدْعُوهُ كَادُوا۟ يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu aliposimama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنَّمَآ أَدْعُوا۟ رَبِّى وَلَآ أُشْرِكُ بِهِۦٓ أَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنِّى لَآ أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنِّى لَن يُجِيرَنِى مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلْتَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا بَلَٰغًا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَٰلَٰتِهِۦ وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوْا۟ مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hata watakapo yaona wanayoahidiwa, ndipo watakapojua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنْ أَدْرِىٓ أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُۥ رَبِّىٓ أَمَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَٰلِمُ ٱلْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِۦٓ أَحَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا مَنِ ٱرْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُۥ يَسْلُكُ مِنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِۦ رَصَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa Mtume wake aliyemridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا۟ رِسَٰلَٰتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَىْءٍ عَدَدًۢا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote waliyo nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Nooh
Sura Al-Muzzammil →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.