Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, “Waonye watu, na wabashirie wale walioamini ya kuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi?” Wakasema makafiri, “Hakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi, anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je, hamkumbuki?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru, wana vinywaji vya maji ya moto, na adhabu chungu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyakufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyelifanya jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo isipokuwa kwa haki. Anazipambanua Ishara kwa kaumu wanaojua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika kuhitilafiana usiku na mchana, na katika vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa kaumu wamchao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wasiotaraji kukutana nasi, na wakaridhia uhai wa dunia hii na wakatua nao, na wale walioghafilika mbali na Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itapita mito kwa chini yao katika Mabustani yenye neema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWito wao humo utakuwa, “Subhanaka Allahumma (Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu!)." Na maamkizi yao humo ni "Salama." Na mwisho wa wito wao ni, “Alhamdulillahi Rabbil 'aalamiin (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote)."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kama Mwenyezi Mungu angeliwafanyia watu haraka kuwaletea maovu kama wanavyojiharakishia kuletewa heri, basi bila ya shaka wangelikwishatimiziwa muda wao. Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtu akiguswa na shida, hutuomba naye ameegesha ubavu, au amekaa au amesimama. Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliviangamiza vizazi vya kabla yenu walipodhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini. Hivyo ndivyo tunavyowalipa kaumu wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawafanya nyinyi ndio wenye kushika pahala pao katika ardhi baada yao ili tuone jinsi mtakavyotenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake? Hakika hawafaulu wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!” Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka mbali na hao wanaomshirikisha nao.”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitilafiana. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hakuna shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika yale wanayohitilafiana.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema, “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Sema, “Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa, tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu. Sema, “Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu wanayaandika hayo mnayoyapangia njama.”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri na wakaufurahia, upepo mkali ukayajia, na yakawajia mawimbi kutokea kila mahali, na wakaona kwamba wameshazingirwa, basi hapo wanamwomba Mwenyezi Mungu kwa kumpwekeshea yeye tu dini, “Ukituokoa kutokana na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini anapowaokoa, tazama, wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mfano wa uhai wa dunia hii ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi ikachanganyika nayo miongoni mwa vile wanavyovila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana. Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu kwa kaumu wanaotafakari.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliochuma mabaya, malipo ya baya ni kwa mfano wake, na watafunikwa na madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao ni kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni. Wao, humo watadumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuko kila nafsi itayajua iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote ya uongo waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti, na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai? Na ni nani anayeyaendesha mambo yote?" Basi watasema, "Mwenyezi Mungu." Basi sema, "Je, hamchi?"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi ni vipi mnageuzwa?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe, kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu anaanzisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha. Basi ni vipi mnadanganywa?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?" Sema, "Mwenyezi Mungu anaongoa kwenye haki." Basi, je, yule anayeongoa kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au yule asiyeongoka isipokuwa akiongozwa? Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Na hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini ni usadikisho wa yale yaliyoitangulia, na ni maelezo ya kina ya Kitabu kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma ndiyo wanasema ameizua? Sema, "Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite muwawezao, kando na Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali waliyakadhibisha yale wasiyoyaelewa elimu yake vyema kabla hayajawajia maelezo yake. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakikukadhibisha, basi sema, "Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza. Je, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Siku atakapowakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana! Watatambuana. Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ima tutakuonyesha baadhi ya yale tunayowaahidi, au tukufishe kabla yake, basi marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayoyafanya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila umma una Mtume. Kwa hivyo, anapowajia Mtume wao, inahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawadhulumiwi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao waliowekewa. Ukifika muda wao, hawakawii hata saa moja wala hawatangulii.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo katika ardhi, basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo. Na watakapoiona adhabu, wataficha majuto. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Yamekwishawajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na ponya ya yale yaliyo katika vifua, na uongofu, na rehema kwa Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Hayo ndiyo bora kuliko hayo wanayoyakusanya."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, mnaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani, wala hamtendi kitendo chochote isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kibainifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWao wana bishara njema katika uhai wa dunia na katika Akhera. Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na wala hawafuati hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu washirika wowote. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawasemi isipokuwa uongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyewawekea usiku ili mtulie humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kaumu wanaosikia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalisema, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana." Ametakasika! Yeye ndiye asiyehitajia kitu. Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Je, mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHiyo ni starehe ya duniani tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Kisha tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wakamkadhibisha. Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio waliobakia, na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha baada yake tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake. Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Je, umetujia ili utuachishe tuliyowakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika ardhi? Wala sisi hatuwaamini nyinyi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walipotupa, Musa akasema: Mliyoleta ndiyo uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Hakika Mwenyezi Mungu hayatengenezi matendo ya waharibifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hawakumwamini Musa isipokuwa baadhi ya vijana kutoka kwa kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika ardhi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa waliopita kiasi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa alisema: Enyi kaumu yangu! Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamteremshia ufunuo (wahyi) Musa na ndugu yake kuwa: Watengenezeeni majumba kaumu yenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndimo mahali pa ibada, na mdumishe Swala, na wape habari njema Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Hivyo wanapoteza watu kutoka kwa njia yako. Mola wetu Mlezi! Zifutilie mbali mali hizo na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka waione adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukawavusha bahari Wana wa Israili, naye Firauni na askari wake wakawafuata kwa dhuluma na uadui. Mpaka kuzama kulipomfikia, akasema: Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLeo basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa wale walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika mbali na Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliwaandalia Wana wa Israili makao mema, na tukawaruzuku katika vitu vizuri. Nao hawakuhitilafiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa uko katika shaka juu ya yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwishakujia haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kwa nini haukuwepo mji ulioamini, kwa hivyo Imani yake ikaufaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa angelitaka Mola wako Mlezi, wangeliamini walio katika ardhi wote kwa pamoja. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haiwi kwa nafsi kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu juu ya wale wasiotumia akili zao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi, je, wanangojea kingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao? Sema: Ngojeni! Nami hakika ni pamoja nanyi katika wanaongoja.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mko katika shaka juu ya Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnaowaabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namwabudu Mwenyezi Mungu anayewafisha. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wala usiombe badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Na ukifanya hivyo, basi wewe hakika ni miongoni mwa madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye. Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake, na Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi watu! Haki imekwishawajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, anayeongoka, basi anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wewe fuata yale yanayofunuliwa kwako kwa ufunuo (wahyi). Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa wanaohukumu.