قُلْ أَرَءَيْتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَٰلًا قُلْ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمْ أَمْ عَلَى ٱللَّهِ تَفْتَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, mnaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: je, mwaonaje zile rizki alizo kutemshieni Mwenyezi Mungu nanyi makafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali Sema: je, Mwenyezi Mungu amekuruhusuni au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu.