وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِ قُلْ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ سُبْحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!” Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka mbali na hao wanaomshirikisha nao.”
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha,na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye.