وَلَوْ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسْتِعْجَالَهُم بِٱلْخَيْرِ لَقُضِىَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا فِى طُغْيَٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kama Mwenyezi Mungu angeliwafanyia watu haraka kuwaletea maovu kama wanavyojiharakishia kuletewa heri, basi bila ya shaka wangelikwishatimiziwa muda wao. Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa lau kama Mwenyezi Mungu angeli wafanyia watu haraka kuwaletea shari kama wanavyo jihimizia kuletewa kheri, bila ya shaka wangelisha timiziwa ajali yao. Lakini tunawaacha wale wasio tumainia kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.