caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Yunus, Aya 27

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 51 · 10:27

وَٱلَّذِينَ كَسَبُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ جَزَآءُ سَيِّئَةٍۭ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ مَّا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ كَأَنَّمَآ أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مُظْلِمًا أُو۟لَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ هُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliochuma mabaya, malipo ya baya ni kwa mfano wake, na watafunikwa na madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao ni kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni. Wao, humo watadumu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70